Mr.Nice akifunguka kuhusu utajiri wake ulivyotoweka ghafla!. Katika hali yakushangaza, Lucas Mkenda au maarufu kama Mr.Nice, finaly afunguka kuhusu utajiri wake na sababu za kushuka kwake kimuziki, katika moja ya interview.
Mr.Nice alidai kuwa hajui ni nini haswa kilichotokea ila yote hayo ni mipango tu ya Mungu. Mr.nice alizidi kufunguka na kusema kuwa, alikuwa na jumla ya zaidi ya shilingi bilioni 1.5 zote zikiwa katika account mbalimbali hapa nchini, na hela zote hizo zimetoweka katika kipindi cha muda mfupi bila yeye kujua zimetumikaje.
“Kaka naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu, kwani sikuwahi kumdhulumu mtu wala kuiba cha mtu, pesa yote nilikuwa naipata kwa hali, naweza kusema hii ni mipango ya Mungu tu wala si mkono wa mtu” alisema Mr.Nice.
“Niliwahi kumiliki zaidi ya milioni elfu moja na mia tano kwenye bank tofauti hapa nchini, pesa hizo zilitokana na kufanya shoo nyingi za nje ya nchi kama. Marekani,Uingereza, Ujerumani, Sweden, Holand, Dubai, SouthAfrica na kwingineko, na kila shoo nilikuwa napata pesa ndefu sana”
Alimalizia star huyo kutoka Tzee na mwanzilishi wa staili ya TAKEU.
Mbali na kushuka kwake kimuziki Mr.Nice anakiri kuwa ana-miss sana enzi hizo kwenye show zake zisizoweza kusahaulika na machozi huwa yanamtoka kila akumbukapo show aliyopiga nchini Rwanda. Ambapo hadi waziri wa nchini humo aliweza kumsubiria airport kumpokea tena kwenye red carpet huku akisindikizwa na magari ya polisi, pamoja na mashabiki wake lukuki waliojaza uwanja huo wa ndege kushuhudia ujio wake..:
Wednesday, July 16, 2014
Tuesday, July 15, 2014
Wednesday, July 2, 2014
Tuesday, July 1, 2014
MIKOA INAYO ONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI TANZANIA.:
MSEMAJI wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Glory Mziray hivi karibuni alisema Mkoa wa Njombe, Mbeya na Iringa ni vinara wanaoongoza kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi nchini.
Alisema Njombe inaongoza kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1 na Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya tatu kwa asilimia 9.
Mikoa mingine na asilimia za maambukizi katika mabano ni Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).
Mikoa mingine aliyoitaja ni Mara (4.5), Mwanza (4.2), Mtwara (4.1), Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8), Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja (1.9) na Pemba (0.3).
Mziray alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo, alisema maambukizi ya Ukimwi yamepungua kwa kasi ndogo.
Alisema Watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi wanafikia asilimia 60 jambo linalosababisha kuwepo mwamko mdogo wa kubadili tabia.
Kuhusu tohara kwa wanaume, alisema inapunguza maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 60 na kusisitiza kuwa ipo haja ya kutoa elimu zaidi juu ya uelewa wa ugonjwa huo
Subscribe to:
Comments (Atom)
MASHINE ZA UMWAGILIAJI
PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44 CONTACT 0685476657

-
Yanga SC imetangaza rasmi kumfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera pamoja na benchi lake lote la ufundi hadi walinzi wa timu hi...
-
MSEMAJI wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Glory Mziray hivi karibuni alisema Mkoa wa Njombe, Mbeya na Iringa ni vinara wanaoo...