Akizungumza na Uwazi, Wolper alisema, amefikia uamuzi huo kwa sababu ana uchungu moyoni unaotokana na dhana waliyonayo wanaume wa Kitanzania juu yao, wakiamini kuwa ni wahuni tu hivyo kuwashusha thamani.
Kule bwana (hajataja nchi) mtu akimuoa staa, anampa kipaumbele. Anaweza hata kutumia fedha kuhakikisha anakuwa na staa na maisha ya mke wake yanakuwa yenye amani lakini hapa kwetu tunadharaulika sana ndiyo maana nimefikia uamuzi huu,” alisema Wolper na kuongeza:
“Unajua
Watanzania wanaamini staa kuandikwa magazetini ni uhuni lakini
wanasahau kuwa maisha yake na magazeti ni kitu cha kawaida kwa sababu
ya kujulikana. Mimi sina haja ya kueleza sana lakini naapa kabisa, mimi
siwezi kuolewa na Mbongo.”
No comments:
Post a Comment