Tuesday, March 18, 2014

Zitto Z. Kabwe na Januari Y. Makamba,mnataka kumpotosha nani?

Wote wawili ni Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba.Wote wawili ni Wabunge vijana kabisa tena wenye uelewa mkubwa. Wote wawili ni Wabunge machachari katika kujenga hoja na kutetea mnachokiamini.Wote wawili ni kati ya Wabunge watumiaji wakubwa wa mitandao na vyombo vingine vya habari. Nyinyi ni mfano wetu sisi vijana katika kuonyesha ya kuwa sisi vijana tunaweza.

Leo, mmechomoza 'twitter' na kuandika maoni yenu juu ya Hotuba ya Jaji Joseph Sinde Warioba alipowasilisha Rasimu ya Katiba Bungeni. Naamini wote mlikuwepo Bungeni na kupata nafasi nzuri na ya mwanzo katika kusikiliza na kuelewa alichokisema Jaji Warioba. Nyinyi mlipaswa kuelewa zaidi na kuja kutuelekeza na sisi. Lakini,mna nia ya kupotosha ukweli.

Wote mnajenga hoja kuwa Jaji Warioba ana nia ya kuuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Mmeitumia Hotuba ya Jaji Warioba kujengea hoja zenu. Ndugu Makamba umekwenda mbali zaidi na kusema kuwa CCM itatumia wingi wake kuulinda Muungano. Unajaribu kuuaminisha umma kuwa Jaji Warioba anatoa hoja ya kuuvunja Muungano uliopo.

Mahali gani aliposema nia ya kuuvunja muungano? Mahali gani aliposema hautaki kuuona wala kuusikia muungano uliopo? Hapa mnajaribu kupotosha.Na hamtaweza. Kwasasa tuna uelewa na ufuatiliaji wa kutosha. Si rahisi kuturubuni na kutupotosha.

Baniani mbaya,kiatu chake dawa!

Mods, tafadhali msiuchanganye uzi huu tukisubiri majibu

No comments:

Post a Comment

MASHINE ZA UMWAGILIAJI

 PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44 CONTACT 0685476657