Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel
Sitta, amejibu mapigo akiwashambulia wasomi wanaohoji uhalali wa wajumbe
wa Bunge hilo kupiga kura wakiwa nje ya nchi, akisema wasomi hao
wanachanganya sheria za nchi.
Sitta aliwafananisha viongozi wa Ukawa na wasanii waigizaji, akitabiri kuwa watashindwa vibaya katika uchaguzi mkuu wa 2015.
Halikadhalika, mwenyekiti huyo ametumia
fursa hiyo ‘kuwapoza’ wajumbe ambao ni waumini wa Dini ya Kiislamu
wanaopaza sauti wakitaka Mahakama ya Kadhi itambuliwe, akisema kuna
‘namna’ itaingizwa kwenye Katiba.
Sitta alitoa matamko hayo mawili jana,
wakati akiendesha vikao vya Bunge hilo mjini Dodoma, katika kipindi
ambacho suala la Mahakama ya Kadhi likiwa limewagawa wajumbe wa Bunge
hilo katika makundi mawili kwa misingi ya imani za dini zao.
Alianza kwa suala la wasomi mbalimbali
wanaohoji uhalali wa Bunge hilo kutaka kuruhusu wajumbe wake watakaokuwa
nje ya nchi, kupiga kura ya uamuzi kupitisha Rasimu ya Katiba
inayopendekezwa akisema:
“Kuna watu wanaojiita wasomi, nadhani
wanaohusiana na hao wanaoitwa Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi) ambao
jitihada yao kubwa sana ni kuzuia kabisa isipatikane katiba.” Sitta
akaongeza kusema, “Leo (jana) nimemsikia mmoja anasema kwamba kupiga
kura (nje) itakuwa sivyo tutakuwa tanavunja katiba ya nchi. Huyu mtu
kasoma sheria ya uchaguzi,” alisema.
Source:Gazeti la Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MASHINE ZA UMWAGILIAJI
PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44 CONTACT 0685476657

-
Yanga SC imetangaza rasmi kumfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera pamoja na benchi lake lote la ufundi hadi walinzi wa timu hi...
-
MSEMAJI wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Glory Mziray hivi karibuni alisema Mkoa wa Njombe, Mbeya na Iringa ni vinara wanaoo...
No comments:
Post a Comment