Serikali imesema kuwa inaendelea kufatilia ili kuchukua hatia zaidi juu
ya matukio yalitokea nchini India katika chuo cha Acharya Bangalore,
ikiwemo la mwanafunzi wa Kike kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agustino Maige
Akitoa tamko la Serikali leo Bunge Mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nchi
za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt.
Agustino Maige amesema tayari serikali imeshapeleka dokezi la
kidiplomasia kwa serikali ya india ili kuonyesha kukasirishwa na kitendo
hicho.
Balozi Maige ameongeza kuwa tayari wameitaka serikali ya India kuchukua
hatua za kipolisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na
kupeleka ulinzi wa kutosha katika maeneo wanaoishi wanafunzi hususani
wa kitanzania ambapo leo kumeri kwa mtu anaesadikiwa kuwa mtanzania
kufariki katika mazingira ya kutatanisha.
Kwa upande wa baadhi ya wabunge wameiomba serikali kuwa na tamko rasmi
la kuonyesha kuchukizwa na ubaguzi kwa watanzania pindi waendapo kuishi
nje ya Tanzania.
Tukio hilo limekuja baada ya Gazeti la Deccan Chronical la Bangalore
kuripoti kuwa tukio hilo limetokea baada ya mwanafunzi raia wa Sudan,
Ismail Mohammed kugonga gari la raia mmoja wa india mkazi wa
Hessaraghata aliekuwa na Mkewe na kusababisha kifo cha mama huyo.
Wakati huo huo Wanaume wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika kumshambulia
na kumvua nguo mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania wamekamatwa, shirika
la habari la AP limeripoti.
Waziri wa mashauri ya kigeni wa India Sushma Swaraj, aliandika kwenye
Twitter kwamba amesikitishwa sana na “kisa hicho cha aibu” kilichotokea
Jumapili eneo la Bangalore
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MASHINE ZA UMWAGILIAJI
PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44 CONTACT 0685476657

-
Yanga SC imetangaza rasmi kumfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera pamoja na benchi lake lote la ufundi hadi walinzi wa timu hi...
-
MSEMAJI wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Glory Mziray hivi karibuni alisema Mkoa wa Njombe, Mbeya na Iringa ni vinara wanaoo...
No comments:
Post a Comment