RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amezua
taharuki mjini leo baada ya kufika katika Tawi la CRDB (Holland
Branch), akiwa kwenye gari binafsi lenye namba T 182 DFQ huku likiwa
halina nembo ya adamu na hawa wala bendera.
Tukio hilo lililochukuwa takribani dakika 25, limetokea majira ya saa
nne asubuhi ya leo jijini Dar es Salaam katika tawi la benki hiyo ambalo
liko katika makutano ya Barabara ya Ohio na Samora bila kutarajiwa.
Mara baada ya Rais Magufuli kufika katika eneo liliko tawi hilo makutano
ya barabara hizo yalifungwa huku ndipo rais aliposhuka kwenye gari na
kuingia ndani ya benki hiyo.
Wakati akikaribia kuingia ndani ilibidi baadhi ya wateja waliokuwa
wakijiandaa kuingia ndani ya benki hiyo wazuiwe kuingia huku huduma
ikiendelea tu kwa wale ambao walikwisha ingia.
Aidha, baada ya kuingia ndani baadhi ya wateja wa tawi hilo na wananchi
wengine walibaki wakishangaa huku wengine wakijiuliza imekuwaje Rais
kuingia benki kwa staili ile kwani baadhi ya wananchi walidai kuwa
hawajaona tukio kama lile kwa marais wote waliopita.
James Charles, ambaye ni dereva wa Texi, alisema baadhi ya wananchi
waliokuwa kwenye eneo hilo baada ya kuona ulinzi unaimalishwa walishtuka
huku wasijue ni nini kinaendelea, hadi pale walipomuona Rais Magufuli
akishuka kwenye gari hali iliyowafanya wafikirie anakwenda kutembelea
ofisi yake ya zamani.
“Lakini kufumba na kufumbua tukamuona anaelekea kwenye benki ya CRDB
tukajiuliza vipi rais leo kaamua kuwa kama mteja hata hivyo hatujui kama
hiyo ilikuwa inawezekana. Lazima kutakuwa na kitu haiwezekani aende
akachukue fedha kwa utaratibu ule ngoja tusubiri tutasikia amefuata
nini,” alisema Charles.
Joyce Godwin ambaye ni mwanafunzi wa chuo kimojawapo cha elimu ya juu,
alisema kuja kwake kumewashtua wafanyakazi wa tawi la benki hiyo kwani
walidhani alikwenda pale kwa ajili ya kutumbua majipu.
“Mimi wakati Rais Magufuli anaingia nilikuwepo ndani kwenye foleni
nikisubiri huduma kwa ujumla kila mmoja wetu alishtuka lakini hatukujua
kilichomleta,”alisema.
Baada ya Rais Magufuli kumaliza kazi yake iliyompeleka alitoka na kuingia kwenye gari huku akiwapungia mkono wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MASHINE ZA UMWAGILIAJI
PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44 CONTACT 0685476657

-
Yanga SC imetangaza rasmi kumfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera pamoja na benchi lake lote la ufundi hadi walinzi wa timu hi...
-
MSEMAJI wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids), Glory Mziray hivi karibuni alisema Mkoa wa Njombe, Mbeya na Iringa ni vinara wanaoo...
No comments:
Post a Comment