Sunday, March 26, 2017

Gari la Uber linalojiendesha lasababisha ajali Marekani

Gari moja linalojiendesha kutoka kampuni ya Uber limepata ajali kwa kugongana na gari lingine huko nchini Marekani katika jimbo la Arizona,
Picha zimeonyesha gari hilo likiwa limepinduka lakini bado hakuna taarifa zozote za majeruhi.
Kituo kimoja cha televisheni kimeripoti kuwa dereva wa gari lililohusika katika ajali na gari la Uber hakuipisha gari hiyo.
Hatahivyo haijulikani iwapo gari hilo la Uber lilikuwa kwenye mfumo wa kuendeshwa bila dereva au la .
Huduma hiyo ya kampuni ya Uber ya magari yanayojiendesha bila dereva ilianza safari zake za uchukuzi mjini Arizona mwezi uliopita, ikiongeza uchukuzi wa safari hiyo kwenye miji mengine kama vile Pittsburgh na San Francisco

Thursday, March 23, 2017

Wafahamu vijana 10 wa chini ya miaka 30 walio matajiri zaidi duniani


Tajiri mmiliki wa ardhi ambaye pia amekuwa akisaidia wasiojiweza katika jamii, Mtawala wa Westminister Gerald Cavendish Grosvenor alipofariki, alimwachia mwanawe Hugh Grosvenor urithi wa £9bn.
Alikuwa na binti watatu, na mwana mmoja pekee wa kiume, Hugh, mwenye umri wa miaka 25.
Hugh alirithi "nusu ya London" kwani ardhi nyingi maeneo mengi ya Belgravia na Mayfair, London ilimilikiwa na babake.
Yeye alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya Bio-bean, kampuni inayoangazia teknolojia isiyoongeza gesi zinazochangia ongezeko la joto duniani.
Kwa mujibu wa orodha ya jarida la Forbes ya mwaka 2016, kuna vijana wengine tisa wa chini ya umri wa miaka 30 ambao utajiri wao ni zaidi ya dola bilioni moja za Marekani.
Vijana wengine matajiri ni:
2 & 3: Alexandra, 20, na Katharina Andresen, 21
Ndio wachanga zaidi na wanamiliki kampuni ya Ferd.
Binti hawa walirithi utajiri hu kutoka kwa baba yao Johan, raia wa Norway mwaka 2007.
4: Gustav Magnar Witzoe, 23
Anatoka Norway pia na huonesha maisha yake ya kifahari kwenye Instagram.
Amerithi sehemu ya biashara ya babake ya kufuga samaki na sasa utajiri wake ni $1.1bn (£846m).
Gustav Witzoe, babake ambaye wana jina sawa, alimpa hisa kwenye kampuni hiyo kama zawadi. Lakini hana udhibiti au usemi wowote.
5&6: Ludwig Theodor Braun na dadake
Haonekani sana mtandaoni. Hayupo kwenye Twitter au Instagram lakini anatambuliwa kwa utajiri.
Familia yake ilianzisha kampuni ya dawa ya B. Braun Melsungen, Ujerumani 1839.
Kampuni hiyo ni maarufu sana kwa dawa na vifaa vya matibabu.
Ludwig humiliki 10% ya kampuni hiyo ambayo ni sawa na $1.8bn (£1.4bn).
Dadake Eva Maria Braun-Luedicke yuko nyuma yake kidogo lakini utajiri wake ni $1.4bn (£1bn).

7&8: Waanzilishi wa Snapchat 

Evan Spiegel ni mmoja wa walioanzisha mtandao wa Snapchat ambao hutumiwa na mamilioni ya vijana duniani.
Majuzi, aliingia uchumba na mwanamitindo mashuhuri duniani Miranda Kerr.


Ana umri wa miaka 26 na utajiri wake ni $2.1bn (£1.6bn), Evan ndiye mchanga zaidi miongoni mwa waanzilishi wa Snapchat na ndiye tajiri zaidi miongoni mwao.
Mwenzake ni Bobby Murphy, 28, ambaye anamkaribia sana kwa utajiri.
Utajiri wa Murphy ni $1.8bn (£1.3bn).
9: Lukas Walton
Kwa mujibu wa Forbes, Lukas Walton, 29, ndiye anayemkaribia sana Hugh Grosvenor.
Utajiri wake ni $10.4bn, ambazo ni karibu £7.2bn kwa viwango vya sasa vya ubadilishanaji wa fedha vya sasa.
Anatoka katika familia tajiri inayomiliki Walmart (miongoni mwa kampuni nyingine), ambayo pia humiliki Asda nchini Uingereza.
10: Wang Han
Wang Han, raia wa China, anakamilisha orodha hii.
Chanzo cha utajiri wake ni urithi wa hisa za kampuni ya ndege ya Juneyao Air kutoka kwa babake Wang Junyao, aliyefariki 2004.
Junyao alikuwa mwanzilishi wa kampuni ya Juneyao Group. Wang Han humiliki 27% ya hisa za shirika hilo la ndege na 14% ya hisa za maduka ya jumla ya Wuxi Commercial Mansion Grand Orient.
Utajiri wake unakadiriwa na Forbes kuwa $1.34bn.


Trump apoteza $800m kipindi cha mwaka mmoja

Mfanyabiashara tajiri wa New York anayewania urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amepoteza $800m ya utajiri wake katika kipindi cha mwaka mmoja, kwa mujibu wa jarida la Forbes.
Jarida hilo linasema kwa sasa utajiri wa Bw Trump ni $3.7bn (£2.7bn).
Forbes wanasema kushuka huko kwa thamani ya utajiri wake kunatokana na 'kudorora kiasi' kwa biashara ya nyumba na ardhi katika soko la New York.
Bw Trump, ambaye wakati mmoja liandika kitabu kwa jina Midas Touch (Mguso wa Midas: Midas aliaminika kubadilisha kila alichogusa kuwa dhahabu), amekuwa akisema kwamba rais wa Marekani kwa sasa anaweza kuwa mtu mwenye busara katika biashara na majadiliano.
Wakati wa mdahalo wa urais Jumatatu, alisema: "Nina mapato makubwa ... wakati umefika kwa taifa hili kuwa na mtu anayefahamu mengi kuhusu pesa."

Alipoteza vipi $800m?
Forbes, ambao wamekuwa wakikadiria utajiri wa Bw Trumo kwa zaidi ya miongo mitatu, wanasema hilo limetokana na kudorora kwa soko la nyumba, afisi na ardhi New York.
Kati ya majumba 28 ambayo yalichunguzwa na Forbes, 18 yalishuka thamani, likiwemo jumba maarufu la Trump Tower linalopatikana Manhattan.
Jumba lake lililo 40 Wall Street na kilabu chake cha Mar-a-Lago kilichopo Palm Beach, Florida, pia vilipoteza thamani, kwa mujibu wa Forbes.
Lakini majumba saba ya Trump, likiwemo jumba la pili kwa urefu San Francisco, yalipanda thamani.

Ametumia pesa ngapi kwenye kampeni?
Inakadiriwa kwamba amewekeza $50m, pesa zake binafsi, kwenye kampeni kufikia sasa.
Forbes wanakadiria kwamba matamshi yake dhidi ya wahamiaji wa Mexico yalimgharimu $100m kupitia mikataba aliyopoteza kwenye mashirika makubwa kama vile NBC Universal, Univision na Macy's.

Utajiri wake kamili?
Utajiri wake kamili haujulikani. Alipowasilisha taarifa zake za kifedha kwa Tume ya Dola ya Uchaguzi, alisema ana "zaidi ya dola bilioni kumi."
Lakini Forbes wanasema utajiri wake ni $3.7bn, Bloomberg wanasema anamiliki $3bn nao Fortune wanasema ana $3.9bn.
Moja ya sababu inayochangia hili ni kwamba Bw Trump pia huhesabu thamani ya jina lake, ambalo anakadiria kwamba thamani yake ni karibu $3.3bn

Mabilionea 25 matajiri zaidi Afrika 2017

1. Aliko Dangote, Nigeria
Utajiri: $12.2 bilioni
2. Nicky Oppenheimer, Afrika Kusini
Utajiri: $7 bilioni
3. Mike Adenuga, Nigeria
Utajiri: $6.1 bilioni
4. Johann Rupert, Afrika Kusini
Utajiri: $6.3 bilioni
5. Nassef Sawiris, Misri
Utajiri: $6.2 bilioni
6. Christoffel Wiese, Afrika Kusini
Utajiri: $5.9 bilioni
7. Nathan Kirsch, Swaziland
Utajiri: $3.9 bilioni
8. Naguib Sawiris, Misri
Utajiri: $3.8 bilioni

9. Isabel dos Santos, Angola

Utajiri: $3.1 bilioni

10. Issad Rebrab, Algeria

Utajiri: $3 bilioni
11. Mohamed Mansour, Misri
Utajiri: $2.7 bilioni
12. Koos Bekker, Afrika Kusini
Utajiri: $2.1 bilioni
13. Allan Gray, Afrika Kusini
Utajiri: $1.99 bilioni
14. Othman Benjelloun, Morocco
Utajiri: $1.9 bilioni
15. Mohamed Al Fayed, Misri
Utajiri: $1.82 bilioni
16. Patrice Motsepe, Afrika Kusini
Utajiri: $1.81 bilioni
17. Yasseen Mansour, Misri
Utajiri: $1.76 bilioni

18. Folorunsho Alakija, Nigeria

Utajiri: $1.61 bilioni
19. Aziz Akhannouch, Morocco
Utajiri: $1.58 bilioni

20. Mohammed Dewji, Tanzania

Utajiri: $1.4 bilioni
21. Stephen Saad, Afrika Kusini
Utajiri: $1.21 bilioni
22. Youssef Mansour, Misri
Utajiri: $1.15 bilioni
23. Onsi Sawiris, Misri
Utajiri: $1.14 bilioni
24. Anas Sefrioui, Misri
Utajiri: $1.06 bilioni
25. Jannie Mouton, Afrika Kusini
Utajiri: $1 bilioni

MASHINE ZA UMWAGILIAJI

 PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44 CONTACT 0685476657