Gari moja linalojiendesha kutoka
kampuni ya Uber limepata ajali kwa kugongana na gari lingine huko nchini
Marekani katika jimbo la Arizona,
Picha zimeonyesha gari hilo likiwa limepinduka lakini bado hakuna taarifa zozote za majeruhi.Kituo kimoja cha televisheni kimeripoti kuwa dereva wa gari lililohusika katika ajali na gari la Uber hakuipisha gari hiyo.
- Mume mzinifu ashtaki Uber
- Uber kutengeza magari yanayoruka
- Uber yatumia ''progamu ya kisiri'' kuhepa wakaguzi
Huduma hiyo ya kampuni ya Uber ya magari yanayojiendesha bila dereva ilianza safari zake za uchukuzi mjini Arizona mwezi uliopita, ikiongeza uchukuzi wa safari hiyo kwenye miji mengine kama vile Pittsburgh na San Francisco
No comments:
Post a Comment