Wednesday, March 8, 2023

MASHINE ZA UMWAGILIAJI


 PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU

TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44

CONTACT 0685476657

Tuesday, November 5, 2019

YANGA YAMTIMUA KOCHA ZAHERA

Yanga SC imetangaza rasmi kumfuta kazi kocha mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera pamoja na benchi lake lote la ufundi hadi walinzi wa timu hiyo, taarifa hiyo imetolewa na mwenyekiti wa Yanga Mshindo Msolla.
Zahera amefutwa kazi Yanga baada ya kuiongoza timu hiyo kwa jumla ya michezo 63 toka alipojiunga na Yanga April 2018, Zahera ameshinda michezo 32 na amepoteza michezo 21 sare mechi 10.
Ndani ya msimu wa 2018/2019 Zahera ameiongoza Yanga kucheza jumla ya michezo 10 na kushinda mitatu, kufungwa 4 na sare michezo mitatu, mkataba wa Zahera na Yanga ulikuwa unamalizika September 2020.

Thursday, May 3, 2018

Mfumo Mpya wa kulipia Bill DAWASCO umeanza kutumika

Leo May 3, 2018 Shirika la Majisafi na Majitaka DSM (DAWASCO), ambapo limesema linatarajia kuokoa takribani Shilingi Milioni 200 kila mwezi, kufuatia kuanza kutumia mfumo mpya wa Kielektroniki wa Malipo wa Serikalini (GePG).
Hayo yamebainishwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASCO, Mhandisi Cyprian Luhemeja ambapo amesema utaratibu huo unaanza leo 

Magufuli: Si wanafunzi wote wa vyuo vikuu watakaopewa mikopo Tanzania

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali ya nchi hiyo haiwezi kutoa mikopo ya kimasomo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu nchini humo.
Kiongozi huyo alisema serikali yake imekuwa ikiongeza fedha za mikopo na kuwakopesha wanafunzi wengi zaidi lakini akasisitiza kuwa sasa haitaweza kutoa mikopo kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu.
"Nataka niwahakikishie Serikali ya Awamu ya Tano inawapenda wanafunzi wa vyuo vikuu, lakini lazima niwaambie ukweli Serikali haiwezi kutoa mikopo kwa wanafunzi wote" alisema.
Dkt Magufuli alisema hayo alipokutana na wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) kilichopo katika Manispaa ya Iringa ambapo alisikiliza kero zao mbalimbali zikiwemo zinazohusu mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na mazingira ya kusomea, kwa mujibu wa taarifa kutoka ikulu.
Rais Magufuli alisema utoaji wa mikopo ya elimu ya juu ni lazima ufuate taratibu pamoja na historia ya familia.
Alidokeza kwamba watakaopewa kipaumbele ni wale wanaosomea udaktari, ualimu na uhandisi.
"Hili suala la mikopo lina changamoto, ndiyo maana tunapotoa mikopo tunaangalia historia ya mtu, ndiyo maana mtoto wangu hapati mkopo," alisema kwa mujibu wa gazeti la kibinafsi la Mwananchi.
"Huwezi kumsomesha mtoto shule ya msingi ya binafsi, halafu baadaye aje aombe mkopo. Hao waliokusomesha wapo wapi? Na kama hawapo tutataka uambatanishe nyaraka kuonyesha hawapo."
Rais huyo alitania kwamba wanawe walijaribu kutumia ujanja wa kutumia jina la mama yao kupata mikopo lakini hawakufanikiwa.
"Hawa majamaa wajanja sana, tulijaribu kutumia jina la mama yao lakini bado wakawagundua," alisema.
Mwishoni mwa mwaka jana, serikali ya Tanzania iliidhinisha Sh427 bilioni za mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/18, lakini viongozi wa wanafunzi walilalamika kuwa bajeti hiyo ilikuwa ndogo ukilinganisha na mahitaji.
Wakizungumza na gazeti hili, baadhi ya viongozi wa wanafunzi walisema bajeti hiyo imekuwa ikizidi kupungua licha ya wanafunzi kuongezeka.
Mkurugenzi wa haki za wanafunzi wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Abdul Nondo aliambia gazeti la Mwananchi wakati huo kwamba bajeti hiyo imekuwa ikizidi kupungua licha ya wanafunzi kuongezeka.
Mwaka 2016/17 serikali ilitenga Sh483 bilioni kwa wanafunzi 120,000 za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu.
"Cha kushangaza mwaka wa masomo 2017/18 wanafunzi wameongezeka na kufikia 122,000, lakini badala ya fedha za mkopo kuongezeka zimepungua na kuwa Sh427 bilioni waombaji wakiwa 61,000 na Serikali imesema itawapa 30,000 pekee," alisema.
Lakini naibu waziri wa Elimu, William Ole Nasha alisema Serikali imetenga fedha hizo kulingana na maombi ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
Alisema: "Kuna vigezo ambavyo vimewekwa na kulingana na vigezo hivyo bodi imejiridhisha fedha hizo zinatosha, bodi ingeomba halafu Serikali ingepunguza lawama hizo zingekuwa na tija.

Sunday, December 10, 2017

Man City imevunja rekodi ya Man United leo

Man City ya Pep Guardiola imefanikiwa kuvunja rekodi ya Man Unired ya Mourinho baada ya kuifunga kwa magoli 2-1, magoli ya Man City yakifungwa na David Silva dakika ya 43 na Otamendi dakika ya 54 wakati goli pekee la Man United likifungwa na Marcus Rashford dakika za nyongeza kipindi cha kwanza.

MASHINE ZA UMWAGILIAJI

 PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44 CONTACT 0685476657