Sunday, March 16, 2014

MAVAZI KATIKA OFISI ZA UMMA-UTUMISHI WATOA MWONGOZO

Wizara ya utumishi wa umma imetuma waraka unaotoa mwongozo wa mavazi kwa watumishi wote wa ofisi za umma na wananchi wote wanaohitaji huduma ktk ofs hizo.
Waraka huo namba 3 wa mwongozo wa mavazi wa mwaka 2007 unawatka wafanyakazi wote wa ofisi za umma na wananchi wote kutokuvaa mavazi yafuatayo:-
-Jeans
-Nguo zenye maandishi yoyote
-Nguo zinazobana mwili wako
-Nguo zilizo juu ya magoti (sketi/gauni)
-Kaptula
-Pedo
-Jezi za timu za mpira
-Nguo za chama chochote cha siasa
-Suruali ambazo hazijapindwa
-Blauz zinazoacha kifua/mgongo wazi
-Kuvaa mlegezo
Waraka huo ulikuwepo ila uekelezaji haukufanyika,hivyo kwanzia mwaka huu utaanza kutumika nchi nzima.
Wananchi usiende ofisi za umma ukiwa umevaa mavazi tajwa hapo juu,utaishia kufukuzwa bila kuhudumiwa...

No comments:

Post a Comment

MASHINE ZA UMWAGILIAJI

 PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44 CONTACT 0685476657