Monday, March 17, 2014

Nimemfumania mke wa rafiki yangu na ameniingizia zaidi ya 1,200,000/= kwa njia ya M-PESA

Katika hali nisioitegemea tumegongana ana kwa ana guest mi na shemeji yangu wa karibu ambae mme wake tunafanya kazi pamoja.

Mimi nikiwa nampeleka mgeni wangu kwenye chumba alichofikia mara ghafla chumba chumba cha pili mlango ulifunguliwa na kikatokea kichwa tu kugeuka tukagongana ana kwa ana huyo shemeji yangu ilichukua takriban sekunde 30 kukodoleana macho na baada kutoa salam sauti ya chini mimi niliingia chumba cha mgeni wangu kumuaga na kumtakia safari njema .

wakati natoka huku mwili ukiwa umekufa ganzi kwa kutoamini nilichokiona kwa shemeji yangu na kutambua alienipokea zamu ya lindo saa 12 jioni mke wake ana madudu niliishiwa nguvu kabisa, alikuja mhudumu wa ile guest akaniitia chemba baadae akaja jamaa ambae sikuweza kumtambua kutokana na mazingira na kunieleza kilichotokea muda mfupi uliopita anaomba iwe niifanye kuwa siri kwanza ametokanae mbali isitoshe ni mzazi mwenzie.

Na akanikabidhi elfu 70 ambayo mi nilikataa kuipokea huku nikimwambia kwasasa nahitaji kuwahi nyumbani mambo mengine tutawasiliana kwa simu ili kukwepa ushaidi niliondoka lakini hatua chache baadae ilipigwa sim kuingalia ilikuwa ya shemeji yangu akinisihi lile suala anaomba liwe siri kwa gharama yoyote ile na nimpe muda mfupi mtu wake anafanya michakato ya hela soon nitapata kwa njia ya M-pesa.

Kubwa kwangu jamaa tumetokanae mbali sana urafiki kwetu ni zaidi ya ndugu tumesoma shule ya msingi moja tumeachana sec. tumeingia depo pamoja na kupangiwa kituo kimoja yaani kama bahati tu hofu yangu ni kwamba asikie hii isue najua alaf sikumpa taarifa atanionaje mimi?

Mpaka sasa natambua kwamba ameoa na ana watoto wawili huyu jamaa ameniambia kwamba ni mzazi mwenzie nashindwa kuelewa na proces zote za uchumba mi nilihusika na sikuambia kama amezaa, katika nyakati tofauti nimeingiziwa kwa mpesa zaidi mil. 1.2 kwa saa 17
nifanyeje?

No comments:

Post a Comment

MASHINE ZA UMWAGILIAJI

 PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44 CONTACT 0685476657