Wednesday, February 10, 2016

Video mpya ya Diamond inaachiwa wiki hii jina la wimbo na aliyeshirikishwa ninazo hapa

Kituo cha Television cha MTV BASE kimepewa tena nafasi ya kuionyesha kwa mara ya kwanza video ya mdundo mpya wa mwimbaji wa bongofleva Tanzania Diamond Platnumz time hii akiwa na rapper wa South Africa AKA na huo mdundo unaitwa ‘MAKE ME SING

Tuesday, February 9, 2016

CHUPA MPYA YA FID Q ft TAZ - WALK IT OFF (OFFICIAL VIDEO) HAAATAREEE

Ahadi ya mabilioni ya Rais Magufuli kwa Mahakama TZ imefanyiwa kazi

Feb 8 2016 Wizara ya Fedha na Mipango ilitoa Bilioni 12.3 kwa ajili shughuli za Mahakama ikiwa ni  utekelezwaji wa ahadi aliyoitoa Rais Magufuli siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya Mahakama  duniani, full stori na makabidhiano yalivyokuwa ndio hii kwenye hii video hapa chini.

Thursday, February 4, 2016

Asking Girls To Be My Girlfriend | Prank | Adrian Gee


Hii video yake mpya Dayna Nyange - Angejua Official Video



Serikali Yazungumzia Tukio la Mwanafunzi wa Kitanzania Kudhalilishwa Kwa Kuvuliwa Mguo Mbele za Watu India.

Serikali imesema kuwa inaendelea kufatilia ili kuchukua hatia zaidi juu ya matukio yalitokea nchini India katika chuo cha Acharya Bangalore, ikiwemo la mwanafunzi wa Kike kudhalilishwa kwa kuvuliwa nguo.

Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agustino Maige

Akitoa tamko la Serikali leo Bunge Mjini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Agustino Maige amesema tayari serikali imeshapeleka dokezi la kidiplomasia kwa serikali ya india ili kuonyesha kukasirishwa na kitendo hicho.

Balozi Maige ameongeza kuwa tayari wameitaka serikali ya India kuchukua hatua za kipolisi kufanya uchunguzi juu ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kupeleka ulinzi wa kutosha katika maeneo wanaoishi wanafunzi hususani wa kitanzania ambapo leo kumeri kwa mtu anaesadikiwa kuwa mtanzania kufariki katika mazingira ya kutatanisha.

Kwa upande wa baadhi ya wabunge wameiomba serikali kuwa na tamko rasmi la kuonyesha kuchukizwa na ubaguzi kwa watanzania pindi waendapo kuishi nje ya Tanzania.

Tukio hilo limekuja baada ya Gazeti la Deccan Chronical la Bangalore kuripoti kuwa tukio hilo limetokea baada ya mwanafunzi raia wa Sudan, Ismail Mohammed kugonga gari la raia mmoja wa india mkazi wa Hessaraghata aliekuwa na Mkewe na kusababisha kifo cha mama huyo.

Wakati huo huo Wanaume wanne wanaotuhumiwa kuhusika katika kumshambulia na kumvua nguo mwanafunzi wa kike kutoka Tanzania wamekamatwa, shirika la habari la AP limeripoti.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa India Sushma Swaraj, aliandika kwenye Twitter kwamba amesikitishwa sana na “kisa hicho cha aibu” kilichotokea Jumapili eneo la Bangalore

MASHINE ZA UMWAGILIAJI

 PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44 CONTACT 0685476657