Friday, July 15, 2016

JUMLA YA OMBAOMBA 60 WAKAMATWA DAR ES SALAAM


Jumla ya ombaomba sitini (60) wamekamatwa katika msako wa ombaomba unaoendelea katika jiji la Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa  na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Grace Magembe alipokuwa akitoa majibu ya uwepo wa ombaomba katika jiji la Dar es Salaam licha ya kuwepo kwa operesheni ya kuwaondoa.

 

 

Pia amesema miongoni mwa ombaomba hao, wapo watoto wenye umri wa chini ya miaka 18   ambao wamepelekwa katika vituo vya watoto yatima, kikiwamo Kituo cha Kurasini.

Dk Magembe amesema  bado ombaomba wamekuwa wakionekana jijini  Dar es Salaam kutokana na kuwapo kwa watu wanaotoka mikoani na kuingia katika makundi ya ombaomba kila siku.

Amesema  uongozi wa mkoa unashirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kutoa elimu mikoani kuhusu operesheni ya kuwaondoa ombaomba.

Amesema ombaomba wengi wanakuja kutoka maeneo mbalimbali ya nchi.

Awali  Makonda alitangaza operesheni kubwa ya kuondoa ombaomba katika Jiji la Dar es Salaam.

aliwataka polisi kwa kushirikiana na ustawi wa jamii kuwaondoa ombaomba wote waliopo mitaani.

Pia, Makonda amepiga marufuku wananchi wanaowapa fedha ombaomba  kuacha mara moja ili wajitafutie riziki wenyewe kwa kufanya biashara au kurudi mikoani kujishughulisha na kilimo.

No comments:

Post a Comment

MASHINE ZA UMWAGILIAJI

 PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44 CONTACT 0685476657