Friday, July 15, 2016

SERIKALI KUWEKA KIPAUMBELE KATIKA KUPUNGUZA VIFO VYA MAMA NAMTOTO NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NCHINI:.

Serikali imesema kuwa itaendelea kuweka kipaumbele cha afya ya mama na mtoto ilikuweza kuondokana na vifo vya mama namtoto ilikuweza kufikia malengo ya milenia ya 2025 yakupunguza vifo vya vitokanavyo afya ya uzazi .

Akizungumza  jijini Dar es salaam waziri wa afya maendeleo yajamii jinsia wazee nawatoto Ummy Mwalimu amesema kuwa sambamba nakuweka kipaumbele kwa afya ya mama namtoto pia ,Serikali itaendelea kutilia msisitizo juu ya utunzaji wa mazingira ilikuweza kuepukana na magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu .

‘’Kila katika mwaka baada yamiezi kumi kumekuwa na ongezeko lawagonjwa wa kipindupindu wapatao 345 nchi nzima,hali hii imechangiwa na hali ya uchafu katika baadhi yamiji yetu ‘’Alisema  Ummy

 

Ummy Mwalimu amesema kuwa jitihada za serikali katika kukomesha mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu haziwezi kufanikiwa endapo serikali hatoweza kuwekeza katika uboreshaji wa mazingira na afya katika maeneo yanayowazunguka wananchi .

Alisema kuwa  serikali inawataka wananchi kutojisaidia ovyo nakudhibiti taka ngumu nakunawa mikono kabla nabaada ya kula chakula.

‘’Hali ya usafi inaimarika katika kipindi cha hivi karibuni baada ya Rais Magufuli kuhimiza wananchi kujenga tabia ya kufanyausafi,lakini hadi hivisasa kunachangamoto ya vifaa vya kuzolea taka ‘’Aliongeza  Ummy Mwalimu


No comments:

Post a Comment

MASHINE ZA UMWAGILIAJI

 PATA MASHINE ZA UMWAGILIAJI KWA BEI NAFUU TUPO SOKO KUU LA KISUTU GOROFA YA TATU DUKA NO 44 CONTACT 0685476657